Model Calisah ambaye anadaiwa kutoka kimapenzi na Wema Sepetu amekataa
kuzungumzia mahusiano yake na Wema Sepetu pamoja na kueleza kwanini
alisema hamjui aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Wema Sepetu na mshindi wa
Big Brother 2014, Idris Sultan.
wema-sepetu-1
Wiki moja iliyopita kupitia kipindi kimoja cha runinga, model huyo alisema hamjui Idris Sultan.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Calisah alisema ni kweli kwamba hamjui
Idris Sultan na wala hakuongea kwa nia mbaya au kutafuta kiki.
“Mimi nashangaa kwanini watu wamepanic kisa kusema simjui Idris Sultan,
kwani yeye ni nani kila mtu amjue?,” aliuliza Model huyo. “Wewe kuna
wanamichezo wangapi wameshachukua tuzo kubwa duniani hawajui?. Kwahiyo
mimi nadhani watu ambao wananishambulia katika mitandao hawajui nini
wanafanya,”
Aliongeza,”Sikusema hivyo kuonyesha dharau, kwa sababu nipo karibu na
Wema lakini hajawai kuniambia kuhusu mtu kama huyo na sijawahi kumuona
naye, na kama ukiwa na mwanamke halafu akawa azungumzia mwanaume
mwingine hizo ni dharau sana. Kwahiyo kiukweli mimi jamaa nimeanza
kumjua baada ya watu kinitag picha zake katika mitandao ya kijamii,”
Pia model huyo alisema kwa sasa hawezi kuweka wazi kama ni kweli anatoka
kimapenzi na Wema Sepetu huku akidai Wema ndiye atayekuwa na jibu
sahihi juu yake.
Saturday, October 29, 2016
Related Posts
UGOMVI wa CUF Wachukua Sura Mpya, Upande wa Lipumba na Maalim Seif Watangaza Kusimamisha Wagombea Kivyao
08 December 2016jimmy lusekelo0BAADA ya Wema Sepetu Kushambuliwa na Mashabiki wa Zari Kuwa Hazai, Aamua Kujibu Mapigo
08 December 2016jimmy lusekelo0CHADEMA wataka Rais Mkapa anyang’anywe shamba kama Sumaye
08 December 2016jimmy lusekelo0Wala Kitimoto Tahadhari: Akutwa na Mnyoo Kwenye Ubongo Wakizani ni Kansa
08 December 2016jimmy lusekelo0
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.