Siku moja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi kutangaza nia ya Serikali kumnyang’anya shamba Waziri
Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, mwanasiasa huyo mkongwe amedai hilo
halimtikisi.
Sumaye ambaye tayari ameshakabidhiwa notisi ya siku 90 kutokana na
kutoliendeleza, amesema kuwa tayari suala hilo ameshaliwasilisha
mahakamani na kwamba mwanasheria wake ndiye anayefahamu tarehe
iliyopangiwa kesi hiyo.
“Nilienda mahakamani na ikaamuriwa kusiwe na shughuli yoyote, nasubiri
tarehe ya kesi ambayo mwanasheria wangu ndiyo anaijua,” Sumaye
anakaririwana MwanahalisiOnline.
Mwanasiasa huyo aliyehamia Chadema miezi michache kabla ya kufanyika kwa
Uchaguzi Mkuu mwaka jana, amesema kuwa kama CCM wanataka kumdhoofisha
kwa kumnyang’anya mashamba ili arejee haitawezekana.
“Kama walidhani kwa kunifanyia hivi nitarudi Chama Cha Mapinduzi (CCM)
wasahau, hata kama nilikuwa na nia hiyo sirudi,” amesema Sumaye.
Serikali imetangaza kuanza mchakato wa kumnyang’anya Sumaye shamba lake
lililoko Mwabwepande jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa ameshindwa
kuliendeleza kwa muda mrefu, kinyume na matakwa ya sheria.
Saturday, October 29, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment