Monday, October 3, 2016

11:22 PM
Sept 21, 2016 majina ya mwanzo ya wasanii watakaowania tuzo za MTV MAMA 2016 yalitajwa huku  Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz na kundi la Navy Kenzo pamoja  na Alikiba ndio wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania tuzo kubwa za Africa za MTV Africa Music Awards 2016.

Sasa basi habari njema leo October 2, 2016 MTV MAMA 2016 wametaja majina mengine ya wasanii watakaowania tuzo hizo ambapo kwa upande wa Tanzania wameongezeka  wasanii watatu akiwemo Raymond wa WCB, Vanessa Mdee na Yamoto Band.

Diamond Platnumz  ametajwa kwa mara ya pili kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Artist of the Year ambacho anachuana na Black Coffee (South Africa), Sauti Sol (Kenya), Yemi Alade (Nigeria), Wizkid (Nigeria).

Mara ya kwanza Diamond Platnumz alitajwa kuwania kipengele cha Best Male ambacho anachuana na Black Coffee (South Africa), Wizkid (Nigeria), AKA (South Africa),  Patoranking (Nigeria).


Vanessa Mdee anawania kipengele kimoja cha Best Female ambacho anachuana na Josey (Ivory Coast), Mz Vee (Ghana), Tiwa Savage (Nigeria), Yemi Alade (Nigeria).

Alikiba ametajwa kwa mara ya pili kuwania kipengele cha Song of the Year kupitia wimbo aliyoshirikishwa na Sauti Sol uitwao Unconditionally Bae.

Kenya imewakilishwa na kundi la Sauti Sol katika  kipengele cha Song of the year na Artist of the year pamoja na Kansoul kwenye kipengele cha Listerners Choice Awards.

 Huku Uganda ikiwa imewakilishwa na wasanii wawili ambao ni Eddy Kenzo  anayewania kipengele cha Best Live Act pamoja na Sheeba anayewania kipengele cha Video of the Year pamoja na Bebe Cool katika kipengele cha Listener’s Choice Awards.

Raymond wa WCB ametajwa kuwania kipengele cha Best Breakthrough Act ambacho anachuana na  Babes Wodumo (South Africa), Emtee (South Africa), Falz (Nigeria), Franko (Cameroon), Nasty C (South Africa), Nathi (South Africa), Simi (Nigeria), Tekno (Nigeria), Ycee (Nigeria).

Yamoto Band wametajwa kuwania kipengele cha Listener’s Choice Awards ambacho wanachuana na Burna Boy (Nigeria), Adiouza (Senegal), Kansoul (Kenya), Meddy (Rwanda), Prince Kaybee (South Africa), Zaho (Algeria), Kiss Daniel (Nigeria), E.L (Ghana), Bebe Cool (Uganda), Latifa (Tunisia), Saad Lamjarred (Morocco), Tamer Hosny (Egypt), Jay Rox (Zambia), The Dogg (Namibia), Sidiki Diabate (Mali), Adiouza (Senegal), Den G (Liberia), Jah Prayzah (Zimbabwe), LIJ Michael (Ethiopia), Messias Maroca (Mozambique).

Hivi ndio vipengele 7  vipya vya wasanii watakaowania  tuzo za MTV MAMA 2016, Jumamosi ya 22 October 2016 kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome Afrika Kusini.

0 comments:

Post a Comment