Meya wa Manispaa ya Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Mendeleo (CHADEMA), Boniface Jacob amemtaka Rais Dk Magufuli kulichukuwa
shamba linalomilikiwa na Rais Mstafuu Mzee Benjamin Mkapa kama
alivyofanya kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Meya huyo alisema kuwa kiongozi huyo wa zamani na familia yake
wanamiliki shamba kubwa katika wilaya ya Ubungo ambalo halijaendelezwa
kwa muda mrefu sasa.
Meya huyo ambaye amekuwa Diwani wa Ubungo kwa muda mrefu ametaa shamba
hilo lililopo Mbezi, Dar es Salaam lirejeshwe kwenye halmashauri ili
liweze kufanyiwa shughuli nyingine.
Hoja hiyo ya Meya wa Kinondoni imekuja siku chache tangu aliyekuwa
Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya tatu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
CHADEMA, Frederick Sumaye aliponyang’anywa shamba lake eneo la
Mabwepande ambalo hajaliendeleza kwa muda.
Meya alitoa maelezo hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la mwananchi
ambapo alisema kuwa watamuandikia Rais Magufuli barua wakimuomba
abatilishe umiliki wa shamba hilo aipe Manispaa ya Ubungo ambayo ndiyo
kwanza imeanzishwa.
Thursday, December 8, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment