Hii hutokea kwa nadra sana na tena kwa wasanii wachache tu wenye ngekewa
zao. Kama ni soka, basi Darassa amepiga hat-trick. Kama Utanipenda, Too
Much na Muziki ni nyimbo zilizobadilisha upepo katika maisha ya muziki
ya Darassa.
Kama Utanipenda na Too Much zilikuwa ni kama mvua za rasha rasha
zilizoashiria kuwa kuna mvua kubwa inataka kunyesha. Bila promo kubwa,
Novemba 23, Darassa aliachia wimbo wake Muziki ambao ungekuja kuwa gia
ya mwisho wa kuashiria kuwa gari limeondoka rasmi.

Naye mrembo mwingine, Elizabeth ‘Lulu’ Michael amepost video akifurahia
wimbo huo na kuandika: Mama Micah on the One n Two…Shikamoo @laviemakeup
Sio Simba,Sio Chui,Sio Mamba….Kazi Yangu Tu inatosha kujigamba
💃Nasikia huu ni Wimbo wa Taifa😝.”
“Mimi Wakazi nasema hivi, Ndio Kwa sasa DARASSA is one of the hottest
rap artist in the country, period. (Nilikuwa Dodoma na Wimbo wake mpya
unafanya vizuri kuliko hata wa Wasafi mpya,” aliandika Wakazi.
Naye producer Jors Bless ameandika: Jamaa ameula bana……. I’m
happy he found a style na sound ya kumtambulisha, you listen to nyimbo
za Darassa from ile alofanya na Blue I think Heya haye or whatever it’s
like from there aliamza kutembea na template ya muziki wake, he found
himself….. That’s what wasanii wengi wanafeli, hawajijui wanafit wapi,
at the end of the day they want to do everything hence a confusion
because there is no identity, darassa found his.”
Ndani ya wiki na nusu, video ya wimbo huu imeshavutia views zaidi ya
788,000 – kitu ambacho ni nadra kwa msanii anayefanya Rap. Umma
umeukubali wimbo huu na ni kweli kuwa kile alichokisema katika miongoni
mwa nyimbo zake za mwanzo kabisa, ‘Sikati Tamaa’ kimemsaidia kufika hapo
alipo leo.
Naamini kuwa Darassa anaelekea kuanza kuifaidi fedha ya muziki ambayo ni
wasanii wachache wapo kwenye nafasi hiyo. Kwakuwa kama alivyosema Jors
Bless kuwa ametambua sound yake, rapper huyu ataendelea kukwea ngazi na
kama ataendelea kutengeneza hits zaidi, Tanzania inaenda kupata msanii
mwingine wa rap mwenye ushawishi mkubwa siku za usoni.
Nauona muziki ukitumika kwenye kampeni na matangazo ya biashara ya
matangazo makubwa. Kwa jinsi wimbo wake unavyofanya vizuri, rapper huyu
hakwepeki kwenye kila tamasha kubwa. Shabiki mmoja anadai kuwa muitikio
wa kushangaza wa wimbo wake, unadhihirisha kuwa woga uliopo kuwa timu
zinadidimiza muziki wa Tanzania hauna maana. Anaamini kuwa kila msanii
atakayeweza kufanya muziki mzuri ana nafasi ya kumega mkate wa tasnia
hiyo.
Tuesday, December 6, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment