Ushindi wa kishindo wa Wizkid kwenye tuzo za MTV MAMA mwaka huu,
unanikumbusha wale wanafunzi wa kiume ambao huwa hawana time kabisa na
wasichana wa darasani, lakini bado watamnasa kila demu mkali.
Wanafunzi wa aina hii ni wale ambao huwa na akili sana darasani au kwao
mambo safi (wana mkwanja) – vitu viwili muhimu vinavyowadatisha madenti
wa kike! Warembo hujipeleka wenyewe!
Tangu kutangazwa kwa majina ya wasanii watakaowania tuzo hizo mwaka huu,
Wizkid hakuwahi kusema chochote. Alikuwa kimya tu utadhani hakuna
kinachoendelea licha ya kuwepo kwenye vipengele vingi.
Hakuwa na muda wa kusema ‘thanks for the nomation.’ Hakuwa na hata muda
wa kusema ‘jama eeh, mwenzenu nimetajwa kwenye MTV MAMA hebu nipigieni
kura.’ He didn’t give a damn! Si ajabu lakini kwasababu ni kawaida yake
bwa’mdogo huyu. Yeye tuzo huziona kitu cha kawaida, mpe sawa, mnyime,
fresh tu!
Ehh! Jumamosi kaibuka na tuzo nne, kawa ‘man of the night.’ Unadhani ni
kura ndizo zimempa ushindi wa tuzo zote hizo? Napata tabu kuamini.
Msanii mmoja mkubwa sana ameniambia, namnukuu: Sometimes KURA
zinapotosha. Watu wamepiga kazi nzuri ila kura zinapick wengine.”
Anachomanisha kuwa, msimamo wa Wizkid kutojishughulisha na kusema lolote
kuhusu tuzo, kunaweza kukawa kulimfanya asipate kura nyingi kihivyo,
lakini ukweli ni kwamba, hakuna msanii Afrika aliyefanya makubwa kumzidi
Wizkid mwaka huu.
Alishirikishwa kwenye wimbo ‘One Dance’ wa Drake ambao umeweka rekodi
kibao ikiwemo ya kusikilizwa mara bilioni 1 kwenye mtandao wa Spotify na
kuwa wa kwanza kuwahi kuvutia namba hizo. Wizkid amefanya kazi na Chris
Brown, Trey Songz, French Montana na wasanii wengine wakubwa. Ndio
msanii anayefanyia kazi Afrika anayefahamika zaidi kwa sasa Marekani.
Hata kama hakuonesha kuzitilia maanani tuzo hizo, ilikuwa ngumu
kumkwepa.
Fundisho hapa ni kwamba, wingi wa kura unaweza usiwe na maana yoyote
katika kumpata mshindi. Haiko sawa kwa namna yake ndio maana Eddy Kenzo
amelalamika. Kwamba kama waandaji wanasisitiza watu wapige kura, lakini
waliopigiwa kura nyingi hawapewi ushindi, ya nini kuwaambia watu wapige
kura? Ni sawa na kampuni kutangaza ajira na kuwafanyia usaili baadhi ya
waombaji huku ikiwa na watu wengine itakaowapa kazi.
Hatuna ulazima wa kujilaumu au kuumia sana au kuushusha muziki wetu.
Wasanii waliotuwakilisha wamefanya kazi kubwa na ngumu kuipeperusha
bendera ya Tanzania. Tusiwabeze, tuwape moyo na kuwaunga mkono bila
kuchoka. Katika kipindi wanachohitaji zaidi support yetu, basi ni hiki.
Friday, October 28, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment