Mashabiki wa Wema Sepetu waushangilia uamuzi huu wa DiamndHakuna kitu ambacho mashabiki wa Wema Sepetu wanakipenda kama kuona kuwa kuna amani kati yake na Diamond.
Pamoja na kuwepo kwa tension kubwa kati ya wawili hao licha ya kila
mmoja kuwa na hamsini zake sasa – yaani Diamond kuhamishia mabaha yake
kwa Zari waliyejaaliwa mtoto wa kike, Tiffah na Wema kuwa mikononi mwa
staa mwenzake, Idris Sultan, mambo yanaonekana kuanza kunyooka.
Jumanne hii Diamond aliwafurahisha sana mashabiki wa Wema pale
alipoipromote show ya Black Tie iliyoandaliwa na Wema na Idris, July 9.
Ikumbukwe kuwa wiki kama tatu zilizopita Wema alisikika kwenye mahojiano
akimtupia lawama ex wake huyo kuwa alimfanyia fitina asiupate ukumbi
kwa King Solomon kwaajili ya show yake hiyo ambapo Christian Bella
atatumbuiza.
Kwa hatua hiyo huenda wawili hao wameamua kuyaacha yapite na wagange yajayo.
Post ya Diamond kuhusu show hiyo tayari imevunja rekodi kwa kuvutia
comments nyingi zaidi. Hadi sasa zimefika takriban 5,000! Comments
nyingi zinampongeza kwa uamuzi huo.
Naye Wema amepost picha mbili zilizokatwa na kuziacha kuanzia kidevuni
kuja chini ambazo zinaonekana wazi kuwa ni picha za Diamond. Wakati
wengi wakifurahia,upande mmoja lakini haujakipokea kikombe hicho cha
chai – Team Zari!
Home
»
Udaku
» » Udaku# » Wema Sepetu » Mashabiki wa Wema Sepetu waushangilia uamuzi huu wa Diamond#kwa habari kamili bofya HAPA>>>>>https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=4087899644516539742#editor/target=post;postID=6744742350781230822
Thursday, July 7, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment