Thursday, July 7, 2016

Aneth Mbilinyi
Asomesha watoto wake, na yeye aamua kuingia darasani
Habari hii nimeipata kutoka gazeti la Mwananchi. Na Tumaini Msowoya

Nimeipenda sana habari hii na nimeona ni vizuri,
UKITAKA kuwazungumzia wanawake waliofanikiwa kiuchumi nchini, bila shaka hutaweza kuacha kumtaja Aneth Mbilinyi.

Mwanamke huyo ambaye ni msambazaji wa maji ya kunywa katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Rukwa, amejizolea sisa kutokana na uwezo wake wa kuendesha biashara kubwa.

Kuna msemo unaosema elimu ni ufunguo wa maisha, kwa mama huyu ni tofauti kidogo yeye hakupata elimu ya darasani lakini yeye anasema hajui kusoma wala kuandika, lakini amepata elimu ya maisha ambayo inamsaidia kuendesha shughuli zake za kila siku.

“Sijawahi kwenda shule hivyo kifupi sijui kusoma wala kuandika, lakini nina uwezo mkubwa wa kuendeleza biashara zangu. Mungu akipenda nitaanza darasa la kwanza wakati wowote,”anasema.

Anasema kabla ya kufikia mafanikio yake biashara, maisha yake yalikuwa magumu kwa sababu haikuwa rahisi kwake kupata ajira hakuwa na elimu ambayo ingemwezesha kufanya hivyo.

Aneth anasema ugumu wa maisha ulimpa changamoto hivyo akatafuta mtaji mdogo na kuanza bishara ya kukopesha vitenge ambayo aliiacha mapema kutokana na wengi kushindwa kumlipa madeni yake hivyo kuua mtaji.

Anasema baada ya kuachana na biashara hiyo alianza kusaga unga wa sembe ambapo alikuwa akiusafirisha jijini Dar es Salaam alikokuwa na wateja wengi.

Hata hivyo,biahsara ya sembe ilimshinda kwani nayo haikumpa mafanikio yoyote kitu kilichomkatisha tamaa na kuamua kuachana nayo.

Mwaka 2000 Aneth alianza kuuza maji ya kunywa ambayo alikuwa akiyafuata katika kijiji cha Kidamali kiwandani kisha kuyasambaza Iringa mjini.

“Uaminifu katika biashara ya maji uliwafanya wamiliki wa kiwanda kunipenda hivyo wakaniongezea mtaji na nikawa na uwezo wa kuyasambaza mkoa mzima, na hapo nikaanza kuona mafanikio makubwa,” anasema.
Anasema kuna wakati alikuwa akipewa mzigo mkubwa wa maji unaozidi milioni 20 na kuusambaza bila hasara yoyote licha ya kuwa hawajahi kuhudhuria darasa lolote.

“Hakuna asiyejua kuhesabu hela, kamwe sijawahi kudhurumiwa kwa sababu nipo makini sana kwenye biashara zangu,” anasema.

Anasema miezi sita baadaye alifanikiwa kununua gari aina ya Fuso ambalo lilimwezesha kusambaza maji kirahisi zaidi tofauti na awali alipokuwa akitumia magari ya kukodi au ya kiwanda hicho.
Kutokana na kuwa makini katika uendeshaji wa bishara zake biasharayake ilizidi kukua na akafanikiwa kushi mashas mazuri pamoja na kuwasomesha watoto wake katika shule nzuri ili wasiishi maisha ya kubahatisha kwa kukosa elimu.

“Nilijibana sana japo faida iliyokuwa ikipatikana kutokana na baishara yangu ilikuwa kubwa, malengo yalianza kutimia taratibu na mpaka sasa namshukuru Mungu kwani namimiliki mamilioni ya fedha bila kuingia darasani, anasema.

Baadaye alinunua malori mengine mawili aina ya scania kwa ajili ya kusiadia kusambazia bidhaa zake.
Mbali na mradi wa kuuza maji, Aneth anamiliki maduka ya vyombo na bidhaa nyingine huku akisema siri kubwa ya mafanikio yake ni Mungu na kujituma.

“Hakuna mafanikio yatakayokufuata mwanamke kama atakaa na kusubiri awezeshwe, lazima tukubali kufanya kazi kama watumwa ili siku moja tuishi maisha ya kifahari,” anasema.

Anasema ingawa hajafikia malengo yake , lakini kwa hapo alipo anamshukuru Mungu kwani tayari amejenga nyumba za kisasa, gari kwa ajili ya usafiri na watoto wake wamesoma.
Bila elimu anawezaje?

“Nikubali nikatae, elimu ni kila kitu, napata shida kwenye kazi zangu kwani huwa nalazimika kukariri mambo kichwani ili nisikosee mahesabu, mfano mzuri ninapoenda benki,” anasema.

Anasema kukariri namba na mambo mengine ya kibiashara vimekuwa vikimsaidia katika biashara zake.
Pamoja na mambo hayo, mwanamke huyo anasema amekuwa akishirikiana na mtoto wake wa kwanza ambaye amehitimu shahada ya Uchumi na bishara Chuo Kikuu cha Tumaini.

“Kwa sababu sikubahatika kusoma, wanangu nimejitahidi kuwasomesha hadi watakaposhindwa ili wasije kuishi maisha ya kubahatisha hasa wakati huu ambapo elimu inaonekana kuwa kila kitu,” anasema.

Hata hivyo, anasema taasisi za fedha zinatakiwa kupunguza masharti ya mikopo ili kumwezesha mwanamke mjasiliamari kumudu kuchukua mikopo hiyo pamoja na kurejesha.

“Mara nyingi taasisi za fedha huhitaji mkopaji awe na mali isiyohamishika kama nyumba ama hati ya kiwanja, sharti hili ni gumu kwa wanawake walio wengi jambo ambalo huwakatisha tamaa wanawake kuchukua mikopo,” anasema.

Anasema alifanikiwa katika biashara yake kwa sababu kiwanda kilimuamini na kuanza kumpa bidhaa kwa kumkopesha, lakini kama isingekuwa hivyo hali ingekuwa tofauti kutokana na ugumu wa mashari ya mikopo.
Anaongeza kuwa taasisi za fedha zina wajibu wa kutoa elimu kwa wanawake wajasiliamari ili kuwawezesha wanawake hao kutambua faida na hasara ya biashara zao.

0 comments:

Post a Comment