WAUZA nyago kwenye video za Kibongo, Lulu Abass ‘Lulu Diva’ na Gift
Stanford ‘Gigy Money’ hivi karibuni wamechimbana mikwara na kupakana
shombo kila mmoja akimuona mwenzake kituko kutokana na maneno
anayoyasikia juu yake.
Ishu nzima ilianza baada ya mwandishi wetu kupata ubuyu kutoka kwa mmoja
wa watu wa karibu wa Lulu Diva kuwa anamhofia Gigy Money kumfunika
katika gemu wanalofanya.
Baada ya mwandishi wetu kupewa ubuyu huo alimwendea hewani Lulu, aliposomewa madai hayo mwanadada huyo alisema;
“Nani kakwambia hivyo? Siwezi kumhofia Gigy kwenye kile ninachokifanya,
hana kitu chochote cha kunifanya nimhofie maana ni mtu wa kawaida sana
kwangu.”
Kwa upande wa Gigy alipotafutwa alisema; “Siwezi kupigizana kelele na
huyo demu, anatafuta kiki kupitia kwangu lakini hawezi kuipata hata kwa
dawa, haniwezi kwa kila kitu, akajipange sana na akae akijua simuogopi.”
Sunday, July 17, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment