Utafiti
umebainisha kwamba kufanya mapenzi angalau mara tatu kwa wiki
kunapunguza uwezekano wa kupatwa Heart Attack (Shambulio la Moyo) kwa
50% ukilinganishwa na yule ambaye anapitisha wiki nzima bila kupiga
mambo yetu. Pia utafiti huo unasisitiza ya kwamba mwenye Kufanya Mapenzi
killa siku anaondoa uwezekano wa kupata Heart Attack kwa Asilimia 100%
ZIJUE FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI
Kiafya
Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema
kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza
kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu
atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.
Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.
Kuongeza mwendo wa damu
Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo
na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya
mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji. Msukumo thabiti wa damu
mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye
mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi
cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na
kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.
Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)
Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol)
nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha
mafuta yenye kileo mwilini.
Kupunguza maumivu
Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini
ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo
hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu
ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa.
Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)Majimaji yanayozalishwa katika tezi
ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo
la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara.
Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.
Kupunguza mfadhaiko wa moyo
Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa
kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye
kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi
mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.
Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen)
Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na
za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo
mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi.
Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za
kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.
Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana
Wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka.
Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo
husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha
mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo
(Cardiovascular).
Hupunguza baridi na mafua
Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa
wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo
Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa.
Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.
NB: Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa
HAYA KWA WANA NDOA FANYENI MAPENZI JAPO KWA WIK MARA 3 MUPATE FAIDA
ZA TENDO LA MAPENZI NDANI YA NDOA. KWA WALE WASIOWA HAWAPATI HIZI FAIDA
SHAURI YENU MSIE OWA OWENI MUPATE FAIDA ZA TENDO LA NDOA
Monday, July 18, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment