Mtanzania Mbwana Samatta bado anaendelea kufanya vizuri na kuzidi
kuaminiwa na kocha wake Peter Maes ambaye kwa sasa amekuwa akimpa nafasi
ya kuanza kikosi cha kwanza na kucheza dakika zote 90, usiku wa July 21
2016 Mbwana Samatta aliichezea KRC Genk mchezo wa pili wa Europa League
dhidi ya Buducnost ya Montenegro.
Genk imecheza mchezo wake wa pili na kulazimishwa kucheza kwa dakika 120
na baadae mikwaju ya penati, dakika 120 zilimalizika kwa Buducnost
kuongoza kwa goli 2-0, goli ambazo zilifungwa na Djalovic dakika ya 2 na
Raickovic dakika ya 40 lakini mchezo uliamuliwa kwa mikwaju ya penati
kutokana na KRC Genk kuibuka na ushindi kama huo katika mchezo wao wa
kwanza.
Katika mikwaju ya penati Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa penati
4-2, penati za ushindi wa Genk zilipigwa na nahodha wao Thomas Buffel,
Heynen, Mbwana Samatta na Walsh, hivyo kwa matokeo hayo sasa Genk
itacheza round ya pili ya Europa League dhidi ya Cork City ya Jamhuri ya
Ireland.
Saturday, July 23, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment