Teknolojia ya simu inaendelea kukua siku baada ya siku, baada ya simu
feki kuzimwa na Mamlaka ya Mawasilinao nchini (TCRA), Tecno Mobile
imetangaza kuzindua simu kali ya CAMON C9 yenye uwezo wa hali ya juu
katika kupiga picha, uwezo wa 4G LTE na teknolojia mbali mbali za
kisasa. Ikiwa simu yako ni miongoni mwa simu zilizofungiwa na TCRA basi
ondoa shaka kwani simu hii mpya kutoka Tecno utaipata kwa gharama nafuu
kabisa.
Tecno Camon C9 inaanza kuuzwa rasmi tarehe 25 Juni 2016. Unaweza kufanya
manunuzi ya awali (pre-order) uwe miongoni wa Watanzania wa awali
kujipatia simu hii. Kufanya manunuzi ya awali tembelea exclusive show
room za Tecno jijini Dar zilizopo City Mall, Clock tower na Mobile plaza
ghorofa ya pili.
Kufanya manunuzi ya awali unahitaji kufanya malipo ya awali ya Tsh.
30,000 ambapo mteja atapata kadi ya “huduma kwa wateja kutoka” Tecno na
kifurushi cha zawadi (gift hamper) za bidhaa kutoka Tecno. Kadi ya
huduma kwa wateja itatumika katika kutengenezewa simu katika duka zetu
za Tecno baada ya kujipatia simu yenyewe.
Mauzo rasmi yanaanza 25 Juni 2016 ambapo watakao kuwa wamefanya
pre-order watatakiwa kukamilisha malipo yao dukani hapo na kisha
kuingizwa moja kwa moja kwenye droo ya kijishindia zawadi mbali mbali.
Zawadi za Droo
Zawadi ya Kwanza: Samsung LED TV yenye thamani ya Milioni 1.6
Zawadi ya pili: Jiko ya kutumia umeme (washindi wawili)
Zawadi ya tatu: Birika linalotumia umeme (washindi wawili)
Na zawadi zingine nyingi
Kila mteja atakaye nunua Tecno C9 Jumamosi katika First sale
itakayofanyka pale City Mall (Showroom inaonekana kwenye picha) atakuwa
mshindi. Baadhi ya sifa za Camon C9 itauzwa katika maduka ya Tecno ikiwa
katika rangi 3 tofauti na hizi ni baadhi ya sifa zake.
Kama mpenzi wa picha Camon C9 imekupa Camera unaihitaji kwani inaweza kutambua sura na kupiga selfie kali hata ukiwa gizani.
Pia Camera yake ina urembo wa kweli (make-up) ambayo itafanya picha zako kuwa na mvuto wa asili kitaalamu imeitwa
Watu 50 ndani ya selfie moja
Inasemekana Tecno Camon C9 ina uwezo wa kujaza watu wengi kwenye selfie
moja zaidi ya simu yoyote duniani. Camera ya C9 inachukua angle kubwa
zaidi hivyo kukuwezesha kupata selfie nzuri hivyo kuchukua watu wengi
zaidi.
Jinsi mpya ya kupiga selfie ukitumia Camera ya kati
Tecno Camon C9 itaondoa issue za selfie kutokuwa kati kwa kutumiacamera
iliyo katikati ya simu ambayo wameita “The Perfect Selfie camera”
Umeshawahi kufikiria macho yanaweza kufungua simu? Camon C9 ina Iris recognition
Sasa hutokuwa sababu ya kuweka password zinazofanana na lugha ya kirumi
kwasababu Tecno imebadilisha mfumo wa namna unaweka neno la siri kwenye
simu kwa kuleta teknolojia mpya ya IRIS recognition ambayo inatumia
macho kufungua simu. Tecno Camon C9 inatumia teknolojia hii kumuwezesha
mmliki wa simu ku-unlock simu kwa kuitizama tu.
Unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno kujua zaidi
Facebook: https://www.facebook.com/TECNOMobileTanzania/?fref=ts
Instagram: https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/
Twitter: https://twitter.com/TECNOMobileTZ
Home
»
Burudani
» Simu Mpya Kutoka Tecno, Camon C9 yatua Dar, Ina Kamera ya Hali ya Juu na Mfumo wa Kufungua Simu Kwa Macho
Tuesday, July 19, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment