Diamond si msanii anayekubali tu kirahisi kitu ambacho anahisi kinaweza
kupoteza wazo lake la awali analoamini kuwa ni muhimu kufanikisha kupata
zao zuri zaidi.
Hanscana amesimulia jinsi staa huyo alivyogoma kuendelea kushoot video
ya wimbo wake na AKA ‘Make Me Sing’ baada ya muongozaji kutaka
kurahisisha mambo:
Kipindi inashutiwa video ya make me sing by @diamondplatnumz nilijifunza
vitu vingi sana ila hiki ni kimoja wapo. Tulitembea umbali kama wa km
300 hivi kwenda ku shoot zile scene Diamond anaimba kwenye white bed afu
kati kati ya pori tupu. Kufika kule jamaa aliyepewa deal ya kuleta bed
akageuza maelezo baada ya kuleta cheupe akaleta cheusi.
Diamond akagoma kushoot alafu zilitumika gharama nyiingi sana kuandaa
production kwaajili ya hiyo scene so isiposhutiwa muda huo ile gharama
yote inakuwa hasara na mbaya zaidi juwa lilikuwa linazama hata wangesema
waende town wakachange ingekuwa nje ya muda na kesho yake ilikuwa
tunarudi Dar kumalizia shots za video ya kama utanipenda.
So ilikuwa no way out Diamond lazima ashoot basi wakaanza kumjaza pale
washoot hivo hivo tu ‘ Diamond aligoma mpaka mwisho alisema huwa siamini
Plan B hata kidogo so i can’t broo. Na wote tukamuona miyeyusho but
baada ya video kutoka nimeona faida ya ubishi wake siku ile.”
Home
»
Burudani
» Soma Jinsi Diamond Alivyotaka Kugoma Kushoot Video ya Make Me Sing Baada ya Hili Kutokea..
Tuesday, July 19, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment