Thursday, July 7, 2016

Jana Nasibu Abdul maarufu Diamond Platnumz alipost picha ya Wema Sepetu katika ukurasa wake wa Instagram akiwataka watu wajitokeze kumsupport katika tamasha. Pamoja na Wema Sepetu, Diamond alimpost pia Idris Sultan na Christian Bella.

Diamond Platnumz aliandika hivi “Make sure ya’ all go Support Christian Bella X Wema Sepetu X Idris Sultan na wengine wakali kibao katika Usiku wa #BlackTie pale King Solomon Hall tareh 9 / 07 /2016!!! It’s all about Black and Everything!”

Hii hapa ndiyo picha iliyowekwa kwenye ukurasa wa Diamond Platnumz
Wema Sepetu alipohojiwa kuhusu kitendo hicho alisema kuwa amefurahi sana na kuona kama kuna mzigo alioutua kwani watu walikuwa wakitumia tofauti zao za kutengenezwa kama faida kwao ili kupata wafuasi (Followers).

Aidha, ameeleza kuwa yeye ni shabiki wa Diamond Platnumz na amekuwa akisikiliza nyimbo zake hata baada ya wao kuachana. Amesema kuachana kwao hakumfanyi asiwe shabiki wake.

Alieleza kuwa kwa muda sasa amekuwa akijizuia kuimba nyimbo za Diamond akiwa kwenye public lakini ameona kuwa anajikomoa yeye mwenyewe kwani akirudi kwenye gari lake huwa anaimba. Kwake amesema kuwa kitendo hicho kinaondoa uongo uliokuwa unasemwa kwamba wawili hao wana bifu zito.
Newer Post
Previous
This is the last post.

0 comments:

Post a Comment