Polisi wenye silaha hivi karibuni wali ka nyumbani kwa msanii nyota,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayeishi Mivumoni Madale na kusitisha
shughuli za burudani zilizokuwa zikiendelea ndani, Risasi Mchanganyiko
limedokezwa.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, shughuli iliyositishwa na polisi
ilikuwa ni ile ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mama mzazi wa mkali
huyo wa muziki, Sanura Kassim ‘Sandra’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita. Ilidaiwa kwamba msanii huyo amekuwa akifanya sherehe mara kwa
mara katika nyumba yake hiyo, hali inayosababisha kero kwa baadhi ya
majirani zake, ambao nao, wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kwa
viongozi wa serikali ya mtaa huo.
Gazeti hili baada ya kuupata ubuyu huo, lilifunga safari hadi nyumbani
kwa msanii huyo na ku kia ofisini kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Mivumoni, Deodatus Kamugisha ambaye baada ya kuulizwa kuhusu kuwepo kwa
tukio hilo la askari kuzima sherehe hiyo, alikiri kuwa ni kweli.
“Nimekuwa nikipata malalamiko ya mara kwa mara kuhusu sherehe za Diamond
kuwa waalikwa wake ni vijana wa kihuni ambao wakija huwa wanavuta bangi
hadharani, wanafunga barabara pamoja na kujisaidia haja ndogo
hovyohovyo maeneo ya nje ya nyumba yake.
“Juzi nilipigiwa simu usiku na majirani zaidi ya sita wakila lamika
kuhusu sauti kubwa ya muziki wa kwenye sherehe ya Diamond, nilimuita
lakini akakaidi, ikabidi niende Kituo cha Polisi cha Wazo na kuchukua
polisi wakiwa na silaha na kwenda kufunga sherehe ile, sheria iko wazi
kuhusu utaratibu wa kupiga muziki maeneo ya baa na majumbani,” alisema
Kamugisha.
Baadhi ya majirani waliozungumza na gazeti hili, walisema kumekuwa na
tabia ya Diamond kufanya sherehe mara kwa mara nyumbani hapo, huku
muziki mkubwa ukipigwa, jambo ambalo kwao ni kero.
“Nachukizwa sana na kelele za Diamond, kwani watu tunashindwa kulala kwa
sababu yeye anafanya sherehe mbona kuna kumbi na hoteli anaweza kwenda
tu, mimi nyumba yangu ni kama kilomita mbili kutoka kwake, lakini
nasikia muziki kwa kero, je walio ubavuni mwake si wanataabika sana!”
alisema mzee mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Gazeti hili lilimtafuta Diamond kwa simu yake mkononi ili kuzungumzia ishu hiyo lakini iliita bila kupokelewa kwa muda wote.
Home
»
»Unlabelled
» 302 ONLINE Home » Diamond Platnumz » jimmy lusekelo » Polisi Wavamia Nyumbani Kwa Diamond Platnumz Usiku... KWA TAARIFA ZAIDI BONYEZA HAPA>>>>>
Thursday, July 14, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment