Siku
chache baada ya kuachana na Nuh Mziwanda, mwanadada Shilole ‘Shishi
Baby’, kupitia account yake ya Instagram ametoa tangazo la kuomba
msaada. Tangazo hili linasema
“Anatafutwa mwalimu wa kingereza mzuri, jamani huu sio utani nipo sirias
naona hali ishakuwa sio hali soon natakiwa kuonaa na Niki Minaji hivyo
lazima nijinoeee, namba ya sm 0653883839“, aliandika Shilole kwenye
ukurasa wake wa instagram
Shilole anafahamika kwa kutojua lugha ya kingereza, hivyo kuwa gumzo
anapoongea lugha hiyo ambayo mara kwa mara huwa anachapia, lakini cha
ajabu yeye mwenyewe huwa anafurahia na hajutii kuzungumza lugha hiyo
ambayo haijui, kama alivyowahi kutamka neno la “I love is my country“,
ambalo lilikuwa maarufu na watu kuvutiwa nalo.
Tuesday, July 19, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment