Mwanamuziki wa Bongo flava asieishiwa vimbwanga mitandao kwa skendo ya
kutoka na vijana wadogo walio chini ya umri wake(Serengeti Boys)
amefunguka na kusema asipangiwe ni nani wa kuwa naye na ataendelea
kutoka na viboi vyake.
Akiongea mbele ya Camera za eNewz, Shilole amesema mashabiki wanahitaji
yeye awe na mzee lakini yeye haoni haja ya kuwa na mzee kwa kuwa
hawawezi ‘kumpetipeti’ na kuwataka wamuache achague anachotaka kwa vile
nyumbani yeye ni Zuwena na jukwaani ni Shilole.
“This is my life, nikiwa nyumbani ni Zuwena na nikiwa kwenye TV ni
Shihi, maisha yangu mimi ya nyumbani au maisha yangu binafsi wao
yasiwahusu sana ninaangalia upendo wangu upo wapi.
Nikisema niangalia mashabiki nini wanacho taka wao wanataka niwe na
mzee, sasa maisha yangu nianze kuwa na mzee nianze kumburuza! mimi
ninahitaji kijana aanze kunipetipeti” Alifunguka Shilole kwa madaha.
Lakini Shilole alimalizia kwa kusema kuwa mpenzi wake mpya wa sasa ni
msanii wa muziki na wala hajawahi kubahatika kuwa na mpenzi ambaye ni
dakitari au mwalimu, bali ana nyota ya kukutana na wasanii tu.
Akifafanua zaidi kwenye muonekano wake katika video ya Rayvan, Shilole
amesema hakuvaa chochote ndani(chupi) zaidi ya ‘night dress’, hivyo
ilimbidi atupie kileo ili aweze kufanya scene hiyo.
Sunday, September 11, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment