Baada ya Mrisho Ngasa kukanyaga ardhi ya Tanzania maswali kwa wadau wa
soka yamekuwa ni kutaka kujua kama mchezaji huyo wa zamani wa Yanga
ataruhusiwa kujiunga na klabu yoyote itakayomuhitaji.
Sports Extra ya Clouds ilimtafuta afisa habari wa TFF Alfred Lucas ili
kujua taratibu na kanuni zikoje endapo kama kuna timu itataka kumsajili
Ngasa kwa ajili ya michuano ya ligi kuu Tanzania bara lakini hata
ikibidi mashindano ya kimataifa.
Lucas amesema Ngasa ananafasi ya kujiunga na timu yeyote itakayomuhitaji
huku usajili huo ukitakiwa kufanywa kabla ya Septembre 6.
“Hata sisi tumeiona taarifa ya Ngasa kuwa hana mkataba tena na Free
State Stars sasa kwa usajili wetu wa hapa nyumbani anaweza akapata
nafasi kwasababu dirisha la usajili la FIFA linafungwa September 6 na
hii lazima ieleweke vizuri sana, kilichofanya Yanga achelewe wakati ule
ni usajili wa ndani kwa maana ya kwamba sisi TFF tulifungua usajili wa
ndani kuanzia 15 June -16 August lakini kwa upande wa kimataifa dirisha
linafungwa September 6”, Alfred Lucas alikaririwa na Clouds FM kupitia
Sports Extra.
“Kwahiyo kama itatokea timu inamtaka kwasababu kama ameshapewa barua ya kuachwa kwaiyo inaweza ikamlinda kufdanyiwa usajili.”
Ngasa amerejea Tanzania September 3 akitokea South Africa ambapo
alivunja mkataba wake na klabu ya Free State Stars inayoshiriki ligi kuu
nchini humo.
Baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa jijini Dar, Ngasa hakuwa tayari
kuzungumza lolote juu ya kuvunja mkataba na kurejea nyumbai badala yake
akasema: “Nimerudi nyumbani kwa sasa imi ni mchezaji huru nimekuja
kupumzika kidogo kisha nitasema nitaenda kucheza wapi.”
Home
»
Burudani
» Mrisho Ngasa Atua Bongo..Hatma Yake Hii Hapa Baada ya Kuvunja Mkataba na Free State
Sunday, September 4, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment