Baada ya hivi karibuni Sholole na Nuh Mziwanda kupatana, Shilole
amefunguka na kuzungumzia nini kimemsukuma mpaka akapatana na mkali huyo
wa wimbo ‘Jike Shupa’.
Wawili hao ambao walikuwa wapenzi waliachana kwa kutupiana maneno huku
Nuh Mziwanda akionekana kumlaumu Shilole kwa kumpotezea muda.
Akiongea na Uhead ya Clouds FM Ijumaa hii, Shilole amedai ameamua
kumaliza tofauti zake na Nuh Mziwanda kwa kuwa muimbaji huyo wa ‘Jike
Shupa’ alikuwa anapoteza kujiamini pale anapokutana naye.
“Nikwambia kitu situation moja ambayo ipo, Nuh akiniona mimi huwa
anapoteza kujiamini,” alisema Shilole. “Sasa ili kumueka sawa na aweze
kuwa vizuri lazima na mimi nimwonesha am good. Kwa hiyo alivyoniona nipo
good na yeye akawa fresh na furaha imerudi na nazani maisha
yanaendelea,”
Hata hivyo mkali huyo wa wimbo ‘Say My Name’ alikanusha kurudiana na Nuh Mziwanda huku akidai kwa sasa wao ni washkaji.
Sunday, September 18, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment