MWISHONI mwa wiki iliyopita (juzi Ijumaa usiku) ilifanyika pati ya
kusherehekea kuzaliwa kwa mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ ambayo imeibua mabifu upya. Pati hiyo
iliyohudhuriwa na mastaa wachache kutoka Bongo ambao ni pamoja na Moze
Iyobo, Aunt Ezekiel na wengineo ilifanyika Zanzibar ambapo licha ya
kufana, imeibua mtifuano upya kati ya Zari na wifi yake, Esma
Abdulkadiri na Diamond na mume wa zamani wa Zari, Ivan Semwanga.
IVAN NA DIAMOND
Bifu la wawili hawa lilikuwa limezimika, lakini lilirudi upya baada ya
juzikati Diamond kumzawadia Zari nyumba iliyopo Afrika Kusini kisha
kumrushia Ivan dongo kwa kuandika mtandaoni: “Wanakazana kujisifu
matajiri ilhali watoto wao wanaishi kwenye nyumba za kupanga… halafu leo
yuleyule wanayemtukana kutwa kwenye mitandao kuwa maskini, kajawa na
shida, kanunua nyumba kulekule kwao ili watoto wao waishi maisha bora
kama wanayoyatamani… Heri ya siku ya kuzaliwa Mama tee wangu…. Nakupenda
sana na unalifahamu hilo…natumai umeipenda nyumba yetu hii mpya South
Africa.”
NI DONGO KWA IVAN
Ujumbe huo moja kwa moja u l i o n e k a n a kumhusu Ivan ambaye kipindi
cha nyuma kwa kushirikiana na mshikaji wake aliyefahamika kwa jina la
King Laurence, walikuwa wakimtusi wakimsema kuwa ni maskini ila wao wana
pesa licha ya madai kuwa, nyumba wanayoishi watoto wa Zari kule Sauzi
ni ya kupanga. Baada ya dongo hilo, hali ilichafuka huku Ivan akimrushia
madongo Diamond sambamba kumtaka Zari amwambie bwana wake (Diamond)
aondoe ujumbe huo mtandaoni kwani hata wanaye wakiuona wataumia.
Inadaiwa kuwa, licha ya Ivan kuomba hivyo, Zari alimjibu kuwa Diamond
amegoma kwa maelezo kwamba, wao (King Laurence na Ivan) ndiyo walioanza
kumtusi.
ESMA NA ZARI
Bifu lao lilihusishwa baada ya Esma kuulizwa sababu za kutomuwish wifi
yake katika siku yake ya kuzaliwa, kuonesha ‘analo na limemfika hapa’
alifunguka: “Siwezi kumuwishi, mbona Taraj (mwanaye) hakumuwishi wakati
ndiye aliyekuwa akicheza na mwanaye (Tiffah) nyumbani? Wee ukosane na
mimi umkasirikie hadi mtoto, ujinga huo. Siwezi kumuwishi Mbona Bi.
Snura (mama wa Diamond) alimuwishi akamfuta na mafumbo juu, akasababisha
watu wakamchamba!….. (anataja jina la mwandishi) nimekaa tumboni kwa
mama yangu miezi 9 ‘so’ mtu anavyomletea dharau siwezi kumpenda. Mbona
wote tumekaa nao vizuri haijawahi tokea haya mambo, kwa nini yeye?”
alihoji Esma.
FAMILIA YA DIAMOND YASUSA BETHIDEI
Katika kile kinachoonesha kuna kitu kizito nyuma ya pazia kati ya Zari
na ndugu wa Diamond, inadaiwa hakuna hata mmoja aliyefika hali iliyoibua
maswali mengi.
DIAMOND, ZARI VIPI?
Kufuatia kuibuka kwa mabifu hayo sambamba na figisu nyingine, gazeti
hili lilifanya jitihada za kuwatafuta Diamond na Zari kupitia simu zao
za mkononi ili waseme lolote, lakini simu zao hazikuweza kupatikana.
Global Publishers
Home
»
Udaku
» >>diamond platnumz>> Familia ya Diamond Yaikacha Sherehe ya Birthday ya Zari Iliyofanyika Zanzibar...Mabifu Yaibuka Upya
Monday, September 26, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment