Msanii Dogo Janja ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kidebe’
na kuwa gumzo mtaani kutokana na kuwasifia baadhi ya wasanii huku
wengine akiwaponda, ambapo ndani yake amemtaja mtu anayeitwa ‘Siwema’.
Dogo janja ametoa ngoma hiyo wakati wimbo wake wa ‘My Life’ ukiwa badi
ni miongoni mwa ngoma ambazo mashabiki wengi wanazikubali huku wengi wao
awali wakidhani kuwa asingeweza kufanya wimbo mwingine zaidi ya huo,
eNewz ilitaka kufahamu kuhusiana na chanzo cha Dogo janja kumsema Siwema
ambaye anajulikana alikuwa ni mpenzi wa rapa Nay Wa Mitego na
kubahatika kuzaa naye mototo mmoja kwa kusema “Siyo kiburi siyo mchafu
kama Siwema” katika ngoma hiyo.
Dogo Janja aliamua kujitetea kuwa Siwema aliyemtaja katika ngoma hiyo
siyo Siwema wa Nay wa Mitego bali ni msichana mwingine kutoka Arusha
mtaa wa Ngarenaro.
Pia alifafanua zaidi kuwa wapo wengi wanaoitwa Dogo Janja lakini sio Dogo janja yeye.
“Mimi sijamzungumzia Siwema wa Nay wa Mitego, Siwema pale mtaani kwetu Ngarenaro kuna mwanamke anaitwa Si
Saturday, September 10, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment