Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
amewapongeza wachezaji wa Timu ya soka ya Wanawake ya Tanzania Bara
(Kilimanjaro Queens) kwa kuandika historia ya kuwa Mabingwa wa kwanza wa
Michuano ya kugombea kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA Challenge) iliyofanyika katika Mji wa Jinja nchini Uganda.
Kilimanjaro
Queens imefanikiwa kutwaa Ubingwa huo baada ya kuibwaga Kenya (Harambee
Starlets) kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika jana
tarehe 20 Septemba, 2016.
Katika pongezi hizo alizozitoa kupitia
kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye, Rais Magufuli amesema Timu ya Kilimanjaro Queens imeandika
historia ambayo inalipa heshima Taifa na inaamsha morali kwa wanamichezo
kufanya vizuri katika mashindano.
“Mhe. Waziri Nape Nnauye
naomba unifikishie pongezi nyingi kwa Wachezaji wa Kilimanjaro Queens,
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Walimu na Viongozi wa Timu pamoja na
wadau wote waliochangia kuiandaa Timu yetu ya Taifa ya wanawake ambayo
hatimaye imepata ubingwa katika michuano hii mikubwa.
“Nimefurahishwa
sana na ubingwa huu na nawaomba wachezaji wa Kilimanjaro Queens na
wanamichezo wengine hapa nchini kuuchukua ushindi huu kama changamoto ya
kuongeza juhudi katika michezo yetu ili nchi isiishie kupata ubingwa wa
Chalenji bali pia ipate ushindi katika michezo na michuano mingine
mingi ambayo hushiriki” Amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli pia
amewaomba Watanzania wote kuendelea kuwaunga mkono wanamichezo na
kuwatia moyo wachezaji kwa kuwa mafanikio yao yanaitangaza nchi na yana
mchango mkubwa katika maendeleo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Thursday, September 22, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment