Msanii wa muziki Barakah Da Prince amekiri kuwa lugha ya Kiingereza
kwake ni tatizo huku akiweka wazi mpango wa kutafuta mwalimu wa
kumfundisha.
Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Nisamehe’ hivi karibuni akiwa
amemshirikisha AliKiba, amesema katika interview yake kubwa iliyopita na
MTV aliomba kutumia lugha ya Kiswahili kwa kuwa ndio lugha ambayo
anaweza kuizungumza.
“Niliulizwa kwenye interview ya MTV kama naweza kuongea Kiingereza,
nilichowajibu naweza ila sio Kiingereza kilichonyooka ndio maana
nikatumia Kiswahili. Nafurahi kwa kuwa walivutiwa na Kiswahili,” Barakah
alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM Jumanne hii.
Pia muimbaji huyo amesema mpenzi wake wa sasa Naj ameshindwa kumfundisha huku akiweka wazi mpango wa kutafuta mwalimu.
“Hanifundishi lugha kwa sababu tuna masihala mengi hivyo nahitaji mtu ambaye atakuwa serious,” alisema Barakah.
Diamond ni miongoni kati ya wasanii ambao walikuwa hawajui kuongea lugha
ya Kiingereza lakini alijifunza na sasa anakichapa kama kawaida.
Home
»
Udaku
» Barakah Da Prince Akiri Kimombo Kwake Bado ni Tatizo, Aanza Mpango wa Kutafuta Mwalimu
Thursday, September 15, 2016
Related Posts
UGOMVI wa CUF Wachukua Sura Mpya, Upande wa Lipumba na Maalim Seif Watangaza Kusimamisha Wagombea Kivyao
08 December 2016jimmy lusekelo0BAADA ya Wema Sepetu Kushambuliwa na Mashabiki wa Zari Kuwa Hazai, Aamua Kujibu Mapigo
08 December 2016jimmy lusekelo0CHADEMA wataka Rais Mkapa anyang’anywe shamba kama Sumaye
08 December 2016jimmy lusekelo0Wala Kitimoto Tahadhari: Akutwa na Mnyoo Kwenye Ubongo Wakizani ni Kansa
08 December 2016jimmy lusekelo0
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.