Mtangazaji wa Clouds FM, Diva The Bawse amewataka mastaa wa Tanzania kutambua thamani ya brand zao na kuacha kujichukulia poa.
Amedai kuwa mastaa wengi wamekuwa wakitumika bure kufaidisha watu wengine na anadhani ni muhimu wakaacha kujishusha kiasi hicho.
Anadai kwa upande wake yeye, hafanyi kitu bure na kudai kuwa hata
kuonekana kwenye saa moja kwenye party ya mtu, ni lazima awe amemlipa.
“My standard rate is 3.5 million in one night that including 30 minutes
hosting, na sikai less than hour naondoka,” Diva ameandika kwenye blog
yake.
“Ifike stage celebs wajue value yao na sio kutumika tu kwa faida ya watu
wengine. Chochote unaona pia napost kwenye account zangu za mitandao
kinalipiwa., lazima ujue kama wewe ni maarufu lazima ulipwe hata kutweet
brand ya mtu mwingine,” ameongeza.
Mtangazaji huyo ana zaidi ya followers milioni 1.1 kwenye Instagram na
amekuwa akiingiza mkwanja mrefu kwa kupost matangazo mbalimbali.
Thursday, September 29, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment