Msanii wa Kundi la muziki la Navy Kenzo, Nahreel amesema ujenzi wa
nyumba yao inayogharimu zaidi milioni 700 unatarajiwa kukamilika mwezi
Disemba mwaka huu.
Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Nahreel amesema anashangaa kuona watu
hawaamini kama pesa zote za ujenzi wa nyumba hiyo zimepatikana kwenye
muziki.
“Watu kuongea ni kawaida lakini mwisho wa siku sisi tunajua pesa zote
zimepatikana kwenye muziki, karibu asilimia 97 ni muziki, kwa hiyo hivyo
ni vitu vya kawaisa,” alisema Nahreel. “Na Mungu akipenda Disemba
mjengo utakuwa umekamilika na kila kitu kinaenda sawa mpaka sasa,”
Pia Nahreel amewataka mashabiki wa muziki wao kukaa mkao wa kula kwa ajili ya video mpya ambayo tayari wameshoot Afrika Kusini.
Monday, September 19, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment