Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize ambaye kwa sasa anafanya
vizuri na wimbo wake wa ‘Matatizo’ amefunguka na kusema kuwa katika
harakati zake za kutafuta maisha alishawahi kuwa dereva wa bodaboda.
Harmonize amesema aliifanya kazi hiyo katika kuhakikisha anaendesha maisha yake kabla ya yeye kutoboa kwenye mambo ya muziki.
Akiongea kupitia kipindi cha ‘Ngazi kwa Ngazi’ kinachorushwa na EATV
Harmonize alisema kuwa anakumbuka mwaka 2011 alikuwa akifanya kazi hiyo
ya kuendesha pikipiki na kubeba abiria ndiyo maana ana uzoefu mzuri wa
kuendesha Pikipiki kutokana na kazi yake hiyo aliyoifanya kwa muda
fulani.
“Unajua mimi nilishawahi kuwa dereva bodaboda nakumbuka ilikuwa mwaka
2011 nilikuwa nafanya kazi ya kubeba watu na Pikipiki hivyo nina uzoefu
mzuri tu wa kuendesha Pikipiki, nilikuwa nabeba abiria hapa na pale
najipatia riziki ndiyo maana hata katika video yangu ya ‘Bado’ niliona
niendesha tu ile pikipiki kwa kuwa nilikuwa na uzoefu wa kuendesha
pikipiki, ” alisema Harmonize
Thursday, September 22, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment