Sunday, September 4, 2016

Licha ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Nigeria, Taifa Stars wamevuna kitita cha dola 10,000 kutoka kwa Gavana wa jimbo la Akwa Ibom State, Udom ambapo ndipo unapopatikana Uwanja wa Uyo uliotumika kwenye mchezo wa jana.

Kitita hicho ni sawa na shilingi za Kitanzania ml 21.7 na Gavana huyo alitoa wakati waliokuwa wakipata chakula cha usiku kwa pamoja baada ya mchezo huo.

Ikumbukwe kuwa katika historia ya timu hizi mbili, Tanzania haijawahi kuifunga Nigeria katika michezo yote waliyowahi kukutana zaidi ya kuambulia vichapo na sare.

Gavana huyo ametoa kiasi hicho cha fedha kutokana na ari ya upiganaji iliyooneshwa na wachezaji wa Stars, ambao walikuwa wakiongozwa na nahodha wao Mbwana Samatta ambaye kabla ya mchezo huo alikuwa gumzo kwa Wanigeria.

Hata hivyo, jana kuna wachezaji ambao walionesha kiwango kikubwa sana kilichowapa mashaka Nigeria. Wachezaji hao ni pamoja na Aishi Manula, Simon Msuva na mabeki wa kati Vincent Andew na David Mwantika.

Vilevile Gavana huyo pia aliwapa Nigeria Naira mil 10 kama pongezi kwa ushindi wao waliopata na kuahidi kuwapa zaidi endapo watafanikiwa kupata nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Russia.

0 comments:

Post a Comment