Anga la burudani nchini hivi sasa lipo kwenye msisimko wa tenzi ya
Wasanii Diamond Platnumz na Raymond ambao wameachia songi la Salome,
ambalo ni marejeo ya songi pendwa lililloimbwa na dada yetu wa Kihaya,
Saida Karoli, liitwalo 'Maria Salome' almaarufu 'Chambua kama karanga'..
Tumeona uongozi wa WCB chini ya Diamond ukijitoa lawama kwa kuonyesha
kuwa kuna makubaliano ya kuurudia huo wimbo baina yao na Dada Saida
kupitia menejiment yake.
Sasa hii ni mara ya 3 huu wimbo unatumika kimaslahi. Mara mbili zote
zilizopita zilionyesha kama dada hakuambilia kitu licha ya watu wa
pembeni kudaiwa kupiga hela ndefu..
Diamond, mshike mkono Saida. Wajanja wasije wakatumia tena ujanja wa makaratasi wakamlaza njaa.
Wednesday, September 21, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment