Hofu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumfutia dhamana Tundu Lissu
ambaye ni mtuhumiwa wa kesi ya uchochezi, imetoweka baada ya mahakama
hiyo kukubaliana na utetezi wa wadhamini wake kuwa, Lissu yupo
Ujerumani kwa matibabu.
Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa jimbo la
Singida Mashariki, alishindwa kuhudhuria mahakamani siku ya juzi na
hivyo wadhamini wake kutakiwa kufika mahakamani jana kujieleza, kwanini
mtuhumiwa huyo asifutiwe dhamana.
Kesi ya uchochezi inayomkabili
Lissu ni kesi Na. 208 katika gazeti la MAWIO akiwa ni mtuhumiwa namba
nne sambamba na Jabir Idrissa, Simon Mkina, na Ismail Merhaboob.
Jabir
ni mwandishi mwandamizi wa MAWIO, Mkina ni mhariri wa gazeti hilo na
Merhaboob ni meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti inayojulikana kwa
jina la Flint.
Jana, wadhamini wa Lissu Ibrahim Ahmed na Robert
Katula walisimama mbele ya Hakimu Thomas Simba anayesimamia kesi hiyo,
na kusema kuwa Lissu hakutokea mahakamani kwa sababu amesafiri nje ya
nchi kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo, upande wa mashitaka
ukiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Mutalemwa Kisheruji uliiomba
mahakama kuzuia hati ya kusafiria ya mshitakiwa Lissu pamoja na
kumuwekea sharti la kuiomba mahakama kibali cha kusafiria endapo
atarudia tena kosa hilo kutokana kwamba hakufuata sheria kwa sababu
alitakiwa kutoa taarifa mapema kabla ya siku ya shtaka kusikilizwa.
Lakini
Hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala na
kuiomba mahakama kutenga siku nyingine ambapo alimuahidi hakimu kuwa
kosa hilo halitajirudia tena na siku husika ya kusikilizwa shitaka
mshatikiwa atakuja mahakamani.
Baada ya kusikiliza maombi ya
pande zote mbili, Hakimu Simba alitoa onyo kali kwa mshitakiwa na
kuwaambia wadhamini wa Lissu kuwa, endapo siku nyingi mshitakiwa huyo
hatakuja mahakamani, wadhamini watalipa dhamana.
Hakimu Simba
aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba, 4, 2016 baada ya mawakili wa pande
zote mbili kuiridhia tarehe hiyo iwe siku ya kusikilizwa shtaka hilo.
Thursday, September 22, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment