Msanii wa muziki AliKiba amempiku Diamond kwa kutoa tsh 21 Milioni kwa
GSM Foundation ikiwa ni siku chake toka muimbaji huyo wa wimbo ‘Kidogo’
kutoa msaada wa tsh 20 Milioni kwa ajili ya kusaidia jitihada za taasisi
hiyo za kutoa huduma ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na
mgongo wazi.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Aje’, ameonyesha kuguswa
na tatizo hilo ambalo limekuwa likiwasababishia watoto ulemavu wa
kudumu.
“Nimeguswa sana na kampeni ya GSM Foundationt katika kuwasaidia watoto
wetu wa Kitanzania wanaosumbuliwa na magonjwa ya kichwa kikubwa na
mgongo wazi. Toka wameanza shughuli hii, mamia ya watoto wameokolewa
kutokana na taabu walizokuwa wanazipata,” aliandika AliKiba kupitia
instagram yake.
Aliongeza, “Nimefurahi kutoa japo kidogo katika niliichojaaliwa kuunga
mkono kampeni hizi.Nawasihi jamii yenye uwezo kila mmoja kwa nafasi yake
kutoa kidogo ili kuokoa maisha ya watanzania.#SupportedByKiba
#KingKiba,”
Kwa upande wa taasisi hiyo, wametoa ujumbe wa shukrani kwa msanii huyo
kwa kuguswa na jitihada za taasisi hiyo za kusaidia watoto aliokatika
wakati mgumu.
“AliKiba tunashukuru sana, kwanza kwa kututembelea katika ofisi yetu ya
#GSMFoundation na pili kwa mchango wako uliotupatia wa kiasi cha
shilingi milioni ishirini na moja (21,000,000) ukiwa ni mchango wako na
kuunga mkono juhudi zetu za kuwafanyia upasuaji watoto wanaosumbuliwa na
magonjwa ya kichwa kikubwa na mgongo wazi. Mwenyezi Mungu akujalie kwa
moyo wako na kukubariki katika kila unalolifanya,” uliandika ukurasa wa
instagram wa taasisi hiyo.
Home
»
Udaku
» AliKiba Atoa Tsh 21M kwa ‘GSM’ Kusaidia Jitihada za Upasuaji wa Vichwa Vikubwa na Mgongo Wazi
Friday, August 12, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment