Gwiji wa mziki wa taarabu nchini Mzee Yusuf amethibitisha kuwa ameachana na kazi hiyo takribani miezi miwili iliyopita.
Taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii zimeeleza kuwa mwanamziki huyo ameachana na mziki na kuamua kumrudia Mungu.
Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu usiku huu, mmiliki
huyo wa bendi ya Jahazi Modern Taarab amethibitisha kuwa taarifa hizo ni
kweli na kuongeza:
“Nashangaa taarifa hizi zinasemwa leo. Ni suala la muda mrefu….takribani
miezi miwili iliyopita na sababu ni kuwa nimeamua kumrudia Allah,”
Mwanamziki huyo mzaliwa wa Zanzibar alipoulizwa kuwa ni suala gani
lililomsukuma hata achukue maamuzi hayo magumu, alijibu kwa kifupi,
“ndivyo tunavyofundishwa na viongozi wa dini.”
Yusuph aliyetamba na vibwagizo kama “Nichumu, nikisi….mwaaaa,” katika
baadhi ya nyimbo zake, amesema familia yake imeupokea uamuzi wake kwa
mtazamo chanya na kwamba inamuunga mkono.
“Kwa sasa nitaimba kaswida zenye mafundisho ya dini,” amesema nyota huo huku akiahidi kufanya mkutano rasmi kuelezea suala hilo.
Mfalme huyo aliyeonekana kuwa ni gwiji wa taarabu ya kisasa (modern
taarab) amezaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1977. Aidha amejihusisha na
sanaa nyingine kama maigizo.
Friday, August 12, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment