Msanii wa muziki Snura Mushi alimaarufu kama Snura Majanga amefunguka na
kusema kuwa amekuwa akipata shida sana na wanaume mbalimbali wenye
matamanio kutokana na vile anavyoweza kutumia mwili wake kwenye uchezaji
wake akiwa stejini.
Snura alizungumza haya kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa
Radio na kusema kuwa licha ya kupata usumbufu huo kwa wanaume hao lakini
amekuwa akijitunza na kujiheshimu kwani anafanya hivyo kulinda kazi
yake na heshima yake kama mwanamke.
"Unajua watu wakisikia Snura Chura huwa wanatokea wengi sana, na kweli
huwa napata shida sana kwa wanaume wengi wenye matamanio, na inawezekana
kweli kati yao wapo wenye mapenzi ya kweli na mimi lakini ndiyo hivyo,
kitu nachozingatia sana ni kuilinda kazi yangu, hivyo wanapotokea
wanaume wa namna hii mimi nachokifanya siku zote ni kuwa mbali nao
kabisa ndiyo maana nashinda vishawishi hivyo kila siku" alisema Snura
Friday, August 12, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment