Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhawani Kikwete amewapongeza wasanii wa
muziki, Diamond Platnumz na AliKiba kwa kutoa msaada wa tsh 41milioni
kwa ‘GSM Foundation’ ili kusaidia jitihada za taasisi hiyo za upasuaji
wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Diamond na Ali Kiba
Mtoto huyo wa Rais mtaafu, amewapongeza wasanii hao kwa kuonyesha kuguswa na kusaidia matatizo ambayo yanatokea katika jamii.
“Katika vitu vimeonyesha umuhimu wa kuwa stars katika jamii yetu ni hili
mlilolifanya wadogo zangu. Ni jambo la kusifiwa na Mungu atawalipa kwa
kuwaongezea maarifa ya kufanya kazi zenu vizuri,” Ridhiwani aliandika
katika instagram yake.
Aliongeza, “Pia niwapongeze sana GSM Foundation kwa kazi nzuri
mnayoifanya. Kutoa si utajiri, ni moyo na mungu atakuzidishia ndugu
mkurugenzi Gharib pale ulipotoa. Kila la kheri katika kusaidia jamii
yetu yenye mahitaji. Peace to you,”
Siku chache zilizopita Diamond Platnumz alitoa msaada kwa taasisi hiyo
wa tsh 20 Milioni na baadae AliKiba na yeye aliamua kutoa tsh 21
Milioni.
Friday, August 12, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment