Wednesday, August 10, 2016

10:08 AM

Jacqueline Wolper amesema anakuja na mradi mkubwa wa fashion huku akidai kuwa ndio kitu anachokipenda zaidi katika maisha yake.

Amedai kuwa kwa sasa yupo kwenye ujenzi mkubwa wa ofisi yake maeneo ya Kinondoni na kwamba akimaliza ataeleza nini hasa anachofungua.

“Sasa hivi nipo kwenye hatua za mwisho, nipo kwenye tiles ndio namalizia kuweka, nikimaliza pale ndio nitawaambia watanzania, mashabiki wangu na wanaopenda kupendeza ni kitu gani nafanya,” ameiambia Bongo5.

Amedai kuwa hiyo ni sababu kubwa imemfanya apumzike kwa muda kwenye filamu kwasababu suala la usambazaji limegeuka kuwa na changamoto.

0 comments:

Post a Comment