Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Geita la
kuwagawia wananchi mabaki ya mawe maarufu kama Magwangala kutoka mgodi
wa dhahabu wa Geita GGM umeanza kutekelezwa.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo yupo katika ziara ya
kikazi katika mgodi huo kwa kutafuta sehemu ambayo wachimbaji watayaweka
na kuyachenjua kwa ajili ya kuyagawa kwa wananchi.
Akiongea mara baada ya ziara hiyo Mhe. Muhongo amesema kuwa agizo la
Rais lilikuwa ni baada ya wiki tatu lakini kwa kuwajali wananchi wa eneo
hilo wameamua kuanza zoezi hilo mapema kwa ajili ya utekelezaji wa
agizo la rais.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Emanuel Kiunga,
amesema kuwa serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na wabunge wa mkoa huo na
baadhi ya viongozi wametafuta maeneo ya kuweka Magwangala hayo kwa
ajili ya kuyahifadhi.
Wakizungumzia maeneo hayo yaliyotengwa kwa ajili ya zoezi hilo baadhi ya
wabunge wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa viti Maalum kwa tiketi ya
CHADEMA, Upendo Peneza, na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku
Musukuma wamesema serikali lazima iwe makini na mawe hayo pamoja na
kuwajali wananchi wa maeneo yaliyotengwa.
Friday, August 12, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment