Msanii wa filamu Faiza Ally amewataka wasichana wenzake kuwakimbia
wanaume ambao wanawataka wasichana ili kufanya nao mapenzi kinyume na
maumbile.
Faiza Ally
Muigizaji huyo ambaye yupo mbioni kuachia filamu yake mpya ‘Baby Mama
Drama’, amewataka wasichana wenzake kuwaepuka wanaume wa nanma hiyo.
“Mtu anayekutaka kinyume na maumbile ni mtu katili sana,” aliandika
Faiza instagram “Wanawake wenzangu msikubali kufanyiwa hivyo, mwananume
anaetaka kukufanyia hivyo ni adui na hana mapenzi zaidi ya kuiridhisha
nafsi yake tu,”
“Na ukikubaliana nae anaona amepata boya, mifano nimeona mingi sana na
wengi wanalia na wamebaki namaumivu na chuki, hata ukinunuliwa gari
halita kuwa milele, hata ukiwa na nyumba hutakula matofali, ukipewa hela
zitaisha, ukipewa kazi mkataba utaisha pia, ukiolewa baada ya muda
utachoka kugeuzwa kila siku na ndoa itakua haina amani moyoni, maana
kigezo sio cha kumpendeza Mungu lakini utu wako utabaki milele,”
alifafanua.
“Pia siku zote usifike mwisho ukakosa plan b siku zote kuna plan
nyingine maana wanawake tunatabia ya kujitolea tupate jambo fulani
lakini si kweli kwamba bila kutoa nyuma utafeli kila sehemu, ukikutana
na jambo kama hili basi acha tafuta kungine ! hakuna kisicho wezekana
haijalishi una haso muda gani, usikubali kuna watu wame haso miaka 30 na
akapata wa 31. Mungu anatoa kwa wakati sahihi,” aliongeza.
Aliongeza,
Monday, August 29, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment