Kitendo cha kocha mpya wa Man United Jose Mourinho kumuingiza Juan Mata
dakika ya 63 na kumtoa katika dakika za nyongeza katika mchezo wa ngao
ya hisani dhidi ya Leicester City, kinaonekana kuchukuliwa tofauti na
kutabiriwa kuwa maisha ya nyota huyo Old Trafford yatakuwa magumu.
Stori kutoka The Times inaripoti kuwa Juan Mata kwa sasa analazimisha
klabu imuachie aondoke licha ya kuwa uongozi wa Man United hawana mpango
wa kumuuza kwa sasa, lakini gazeti hilo pia linaripoti kuwa kocha wa
Everton Ronald Koeman kaonesha dhamira ya kumuhitaji staa huyo.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri suala la Juan Mata kuhusishwa kuondoka
linatarajiwa kutokea kutokana na Jose Mourinho kudaiwa kutomuhitaji,
hali kama hiyo iliwahi kumkuta Juan Mata wakati yupo Chelsea na Jose
Mourinho ila mwaka 2014 aliamua kuondoka klabu hiyo na kujiunga na Man
United.
Friday, August 12, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment