Msanii hip hop hapa nchini, Witness aka Kibonge Mwepesi, ameitaja sababu
ya kujichora tattoo ya jina la mpenzi wake Ochu Sheggy kwenye kiuno
chake.
Akiongea katika kipindi cha E-News cha East Africa TV, Witness amesema ameamua kufanya hivyo ili kuepuka kumsaliti mpenzi wake.
“Ukiweka tattoo sehemu kama niliyoweka mimi(kiunoni) inazuia, hata
unapotaka kumsaliti mwenza wako yule unayekuwa naye inamnyima hamu
kabisa na anashindwa hata kukutamani tena,” alisema Witness.
Pia Witness alisema kuwa watu wanadhani kuwa kuolewa ndiyo kumaliza kila
kitu lakini kwa sehemu ambayo mapenzi yao yamefikia hakuna kitu ambacho
anakihitaji tena kwakuwa mapenzi ni kuungana mkono na Ochu anamsaidia
katika kila kitu anachofanya.
Thursday, August 25, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment