Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diamond Platnumz
amesema anafanya hivyo kwa Chid Benz kutokana na kitendo alichomuonyesha
kabla hajawa maarufu, kukubali kufanya naye collabo ya wimbo wa ‘nalia
na mengi’, bila kumzungusha na kumtoza hela kama ilivyo kwa wasanii
wengine.
“Mimi nimefanya collabo na Chid, kipindi hicho nilimwambia, hakunitoza
hata sh. kumi wala hakunizungusha hata kidogo, ndio maana linapokuja
suala la Chidi nakuwa wa kwanza, wakati mimi namfuata Chidi, Chidi hasa
nikajua atanikatalia kwanza mimi mbana pua, lakini hakunizungusha na
wala hakuniomba hata mia”, alisema Diamond Platnumz.
Tujikumbushe hivi karibuni msanii Chid Benzi alipata matatizo ya
matumizi ya madawa ya kulevya, na Diamond alichukua jukumu la kumpeleka
hospitali na kumbadilisha damu, kabla hajapelekwa rehab kupata tiba ya
urahibu.
Sunday, August 7, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment