MREMBO ambaye jina lake liko juu kwa sasa kwenye gemu la Muziki wa Bongo
Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ hivi karibuni amewaka baada ya kubanwa
maswali juu ya tetesi za uhusiano wake na Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo,
Juma Mchopanga ‘Jay Moe’.
Akistorisha na Uwazi Showbiz, Shilole alifunguka kuwa hana uhusiano na
mkali huyo wa ngoma ya Pesa Madafu na hajawahi kufikiria kutoka naye na
anawashangaa watu wanaomhusisha kuwa kwenye mahaba na Jay Moe.
“Watu bwana wanashindwa kufuata yao wanakalia kuchonga yawenzao, mimi
Jay Moe ni kaka yangu, tumeshibana na hatuna uhusiano wowote,” alisema
Shilole.
Kwa upande wa Jay Moe amefunguka kupitia kwenye mitandao ya kijamii juu
ya kuzisikia tetesi za yeye kutoka kimapenzi na Shilole, amedai pia
hazina ukweli wowote maana mwanadada huyo ni mshikaji wake wa karibu tu!
Tuesday, August 9, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment