Friday, August 19, 2016

11:48 PM
Peter Msechu amefunguka juu ya tuhuma za msanii mwenzake AT aliyedai kumzungumzia juu ya wembamba wake.

Amedai kuwa kwa mtazamo wake hajui nani amemlisha sumu msanii mwenzake huyo lakini ameona ujumbe huo unaodai kuwa anapofanya interview amekuwa akimzungumzia kitu ambacho ni uongo.

“Mara nyingi napofanya interview nimekuwa nikiulizwa kuhusu unene wangu lakini nitakapotolea mfano wa mtu yeyote ambaye ni mwembamba kwenye muziki si mbaya,” ameiambia Bongo5.

“Kuna kipindi nilikutana naye tukafanya interview pamoja na tukataniana lakini nafikiri yeye alichukia binafsi tu lakini nafikiria ilikuwa ni namna ya kutafuta atention tu,” ameongeza.

Hata hivyo Peter Msechu amedai kuwa hajawahi kumtaja AT kwenye interview yake yoyote na wala hajawahi kuwa na urafiki na msanii huyo.

0 comments:

Post a Comment