Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga SC,
wametupwa nje kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada
ya TP Mazembe kuchapwa mabao 3-2 na Medeama ya Ghana katika mchezo wa
kundi A uliofanyika kunako dimba la Essipong Sports huko Takoradi,
Ghana.
Medeama walipata mabao yao kupitia kwa Enock Atta Agyei, Moses Amponsah
Sarpong na Kwesi Donsu huku Mazembe wakipata mabao yao yote mawili
kupitia kwa Jonathan Bolingi.
Kufuatia matokeo hayo, Medeama ambao mchezo wa mwisho watacheza na MO
Bejaia watahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua ya nusu fainali,
wakati huo Yanga watakuwa ugenini wakikipiga na TP Mazembe mjini
Lubumbashi, mchezo ambao utakuwa ni wa kukamilisha ratiba tu kwa upande
wa Yanga.
Mpaka sasa, TP Mazembe bado wako kileleni na pointi zao 10 baada ya
michezo mitano, wakishinda mara tatu, sare mara moja na kufungwa mara
moja, wakifuatiwa kwa karibu na Medeama wenye alama nane, Bejaia
wakishika nafasi ya tatu na pointi zao tano na Yanga wakiburuza mkia na
pointi zao nne.
Hata kama Yanga itashinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mazembe,
haitasaidia chochote katika kufuzu hatua ya nusu fainali kwasababu
watafikisha pointi saba wakiwa wamemaliza mechi zote wakati Medeama
tayari wamefikisha pointi nane ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga.
Mchuano mkali umebaki kati ya Medeama na Bejaia mabapo kila timu inasaka
nafasi ya kuungana na Mazembe kuelekea nusu fainali huku Mazembe pia
ikihitaji kushinda ili kuongoza Kundi lao la A.
Home
»
Burudani
» » yanga » Yanga Yatupwa Nje ya Michuano ya CAF Baada ya Medeama Kuifunga TP Mazembe Usiku wa Jana
Monday, August 15, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment