Mrembo kutokea pande za Mombasa nchini kenya, Vera Sidika ametoa sababu
ya kuwa na bifu na mlimbwende mwenzake wa nchini humo, Huddah Monroe,
bifu ambalo limeteka vyombo vya habari kwa muda mrefu
Akifunguka kwenye FNL ya East Africa Tv na Radio, Vera Sidika amesema
wakati yeye akiwa Mombasa, Huddah Monroe tayari alishakuwa maarufu
jijini Nairobi, lakini alipoenda ingawa walianza kwa kuwa marafiki,
lakini baadaye Huddah alionyesha kutopenda uwepo wa Vera jijini Nairobi,
kwani alihisi anamchukulia nafasi yake kwenye kazi.
"Bifu ambayo yeye anayo ilikuwa yeye amekuwa Nairobi na tayari
alishakuwa star, na mimi nikatoka Mombasa nikaja Nairobi, ikawa kama
nimeingilia career yake, ikawa anaaza bifu leo, anaanza kesho sasa
inachosha, sasa mi nasemaga mambo kama hayo sitaki lakini anayaleta tu",
alisema Vera Sidika.
Vera aliendelea kusema kuwa kitendo hicho yeye hakipendi, hasa pale
inapofikia hatua ya kuchafuana kwenye mitandao kwa kutoleana habari za
uongo, akitolea mfano wa hivi karibuni wa Hudda kumtangaza kuwa yeye ni
muathirika wa Ukimwi.
Home
»
»Unlabelled
» Hiki Ndicho Chanzo Cha Bifu la Vera na Huddah
Sunday, August 14, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment