Tangu malkia wa filamu nchini, Wema Sepetu aachane na mpenzi wake Idris
Sutlan kuna mengi yamekuwa yakizungumzwa katika mitandao ya kijamii.
Muigizaji huyo hakuwahi kuzungumza sababu ya kuachana na mshindi huyo wa
shindano la Big Brother Africa Hotshots 2014 hali ambayo imekuwa
ikiibua maswali mengi kwa mashabiki wake.
Alhamisi hii Wema amewataka mashabiki wake katika mitandao ya kijamii
kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kuyasikia mengi ambayo yanaukabili moyo
wake.
“Kuna muda mtu unaweza ukakaa na ukasema na moyo wako, Ila moyo mara
nyingi huwa unazidi nguvu nyingine zozote. Kuna kitu kiukweli ninacho
kwa moyo wangu,” aliandika mwigizaji huyo kupitia ukurasa wa instagram.
Aliongeza, “Lakini siwezi kusema leo wala kesho, but ipo siku isiyo na
jina wala tarehe nitakisema tu, maana mnanijua kukalfisha nafsi huwa
sipendi, but all in all tuseme Inshallah,”
Wiki iliyopita aliyekuwa mpenzi wake, Idris Sultan aliamua kufuta
akaunti yake ya instagram yenye followers zaidi ya milioni 1 baada ya
kushindwa kuvumilia yale yanayoendelea katika mitandao ya kijamii
Friday, August 26, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment