Msanii wa muziki Diamond Platnumz ametoa msaada wa Tsh 20 Milioni kwa
‘GSM Foundation’ kwa ajili ya kusaidia jitihada za taasisi hiyo ya kutoa
huduma ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI)
kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na GSM Foundation
imekuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya
kutoa huduma hiyo bila gharama yoyote.
Raisi huyo wa label ya ‘WCB’ ameonyesha kuguswa na jitihada za taasisi hiyo na kuamua kuchangiia kiasi hicho.“Moyo wangu unaniambia nisingeshikwa mkono ama kusaidiwa na watu basi
nami nisingeweza leo hii kufikia hatua hii ndogo niliofikia na ndio
maana kidogo nikipatacho huwa napenda kusaidia wenzangu,” aliandika
Diamond Istagram. “Leo Mapema nilitembelea ofisi za GSM foundation
kuwasilisha kidogo tulichobarikiwa kwa niaba ya WCB. kwajili ya kusaidia
watoto wenye matatizo ya Vichwa vikubwa (Bobble Head Syndrome) na
Mgongo wazi,”
Kwa upande wa GSM Foundation, ameandika:"Leo tumepokea hundi ya
shilingi milioni ishirini (20,000,000/=) kutoka kwa @diamondplatnumz
kama mchango wake kwa #GSMFoundation. Tunamshukuru kwa kuja kututembelea
ofisini kwetu na kwa msaada aliotupatia. Mwenyezi Mungu amuongezee pale
alipopunguza
0 comments:
Post a Comment