Hakuna ubishi kuwa mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ ni mjamzito lakini habari ambayo
hujaisikia ni kwamba hivi karibuni mwanamama huyo alidaiwa kutaka
kuichoropoa mimba hiyo.
Chanzo chetu ambacho ni rafiki wa karibu wa Diamond kilitumwagia
ubuyu kuwa, baada ya yale madai kuwa Diamond anatoka na yule Video Queen
wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Irene Hilary ’Lynn’, Zari alimaindi
kinoma na kufikia hatua ya kutaka kuitoa mimba ili kumkomoa Diamond.
Inadaiwa kuwa, kilichomkasirisha zaidi Zari ni kitendo cha mama wa
Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kuonesha kufurahia kitendo cha mwanaye
kumsaliti.
“Ninyi hamjui tu jinsi ile skendo ya Diamond kutoka na Lynn
ilivyotaka kuleta balaa, unaambiwa Zari alitishia kutoa mimba, mbaya
zaidi ni pale zilipoibuka tena taarifa kuwa, Lynn ana mimba, mbona
ulikuwa mtiti?” kilidai chanzo hicho.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa, kutokana na hali hiyo, Diamond alitumia
nguvu kubwa kumsihi mzazi mwenzake huyo kutosikiliza maneno ya watu na
badala yake aitunze mimba hiyo ili amzalie mtoto wa pili baada ya Tiffah
ambaye sasa ana umri wa mwaka mmoja.
Madai hayo yalimfanya paparazi wetu amtafute Diamond ‘Baba Tiffah’
kwa njia ya simu kuyazungumzia ambapo alipopatikana alisema: “Unajua
uhusiano unachangamoto nyingi sana lakini ninachoweza kushukuru ni
kwamba leo hii mimba ya baby wangu ina zaidi ya miezi minne na Mungu
akijaalia mwezi Desemba nitapata mtoto mwingine wa kiume, hayo mengine
tuyaache.”
Akaongeza: “Unajua watu wanaongea sana hasa kwenye mitandao ya
kijamii lakini sisi ni waelewa na hatuwezi kuwapa watu nafasi
watuharibie.”
Diamond na Zari wamekuwa kwenye uhusiano wenye figisu nyingi huku
wengine wakidai hawawezi kudumu kutokana na msanii huyo kudaiwa mara
kadhaa kusaliti ambapo skendo mbichi inayomtafuna ni ya kuwapachika
mimba Lynn na modo Hamisa Mobeto.
0 comments:
Post a Comment