Msanii wa Bongo Movie Wastara Juma amepinga uvumi wa kutoka kwa baadhi
ya watu ambao wamekuwa wanamzushia kwamba yeye ni mjamzito.
Akiongea kwenye kipindi cha eNewz kinacho onyeshwa katika runinga ya
EATV kila siku saa kumi na mbili, Wastara amewaambia wananchi kwamba
tumbo la mimba hukua na halirudi ndani kwa hiyo waendelee kusubiri miezi
tisa mpaka itimie kwani kwanzia waanze kusema yeye ni mjamzito ni miezi
mine na tumbo haliendelei.
Licha ya hilo Wastara amesema tumbo hilo ambalo walikuwa wanalihisi kuwa
ni kijacho, ni kwamba aliridhika tuu na sehemu ambayo alikuwa, kwani
alikuwa Msumbiji kibiashara kwa hivyo mazingira hayo yalimfanya kuwa na
tumbo kubwa na hivi sasa yupo kwenye diet ili kupunguza mwili.
"Unajua kinachonishangaza ni pale wale wanaposema mimi ni mjamzito na
haelewi baba kijacho ni yupi kama ni yule wa ndoa ama ?," alisema
Wastara Juma.
Friday, August 19, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment