Tuesday, August 9, 2016

Ubuyu wa mjini unanyetisha kuwa, mkali wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Jike Shupa aliomshirikisha Ali Kiba, Natfal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anadaiwa kupora demu wa jamaa ambaye naye ni msanii wa wa Bongo Fleva, Valentino Michael ‘Vale wel’.
Mrembo anayedaiwa kuporwa kwa Vale ni yule Nawali ambaye kwa sasa Nuh anamnadi kuwa ni mpenzi wake wa kiyama.

Ubuyu ulionaswa na Wikienda ulidadavua kuwa mwenye demu wake alipigwa na butwaa alipomuona Nuh akimnadi Nawali kwenye mitandao ya kijamii ndipo akang’atwa sikio kuwa kwa sasa hana chake kwani ‘mtoto’ yupo mikononi mwa Nuh.

Akimwaga chozi mbele ya Wikienda, Vale alisema kuwa mpaka sasa hajaelewa ni kwa nini Nuh ameamua kumtangaza Nawali kuwa ni mpenzi wake wakati akijua wazi kwamba ni shemeji yake na ni mwanamke wake wa siku nyingi kwani wanafahamiana.

“Kiukweli nilikuwa sijui hili wala lile. Nilipoingia mitandaoni nilipigwa na butwaa kumuona Nuh akijitangazia ufalme kuwa mpenzi wake kwa sasa ni Nawali.
“Mwanzoni nilijua labda ni mambo ya kiki kwa sababu nijuavyo Nuh hana malengo mazuri na Nawali.

“Baadaye ndipo nikawa nahakikishiwa na watu wangu wa karibu kuwa ni wapenzi na hawafanyi kificho.
“Kinachoniumiza nilikuwa sina tatizo wala ugomvi wowote na Nawali na bado naamini ni mpenzi wangu kwa sababu hatujaachana na tukikutana huwa tuko kama kawaida,” alisema Vale.

MWENYE KISU KIKALI?
Vale alizidi kutokwa povu kuwa kwa sasa hasemi sana kwa sababu hana mkwanja wa kumpa Nawali hivyo ule usemi wa mwenye kisu kikali unamtafuna kwani inawezekana Nuh anatumia vijisenti alivyonavyo kumnyang’anya tonge mdomoni.

“Lakini ukweli ni kwamba ‘nafaiti’ na mambo yatakaponinyookea nitahakikisha nafanya kila njia kumrudisha Nawali kwenye himaya yangu kwani ndiye mwanamke wa maisha yangu.

“Najua nilipomtoa, ni mwanamke ambaye ninampenda sana na nimetumia muda mwingi kumbadilisha kimuonekano kwani mwanzoni hakuwa alivyo sasa, alikuwa mgumu hivyo nimefanya jitihada za hali ya juu kumfanya aonekane ‘soft’,” alimalizia Vale.
Mwanaume anayedai kuibiwa akiwa na niwale enzi zao

HUYU HAPA MTUHUMIWA NUH
Baada ya ubuyu huo ulionyooka kutua kwenye Wikienda, waandishi wetu walimweka ‘mtukati’ Nuh aliyedai kuwa hapendi kumuongelea mpenzi wake huyo kwa sababu kama ni maneno yameshasemwa mengi.

“Unajua kuhusu huyu demu wangu, maneno mengi sana yamesemwa hadi nimechoka. Kama huyo mwanaume yupo na anaamini ni mwanamke wake basi amchukue akakae naye,” alisema Nuh akiomba kuachwa atulize mawazo.

NAWALI ANASEMAJE?
Kwa upande wake Nawali, alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa hamjui Vale na wala hajawahi kupiga naye picha za kimahaba ambazo gazeti hili lina nakala zake.

Habari kutoka kwa Wana-Ubuyu wanaolinyaka vilivyo sakata hilo wanadai kwamba Vale ana uhakika kuwa huyo ni mpenzi wake na picha ametoa wakiwa wawili tena kimahaba hivyo inakuwaje Nawali anabisha?

HUYU NDIYE NUH
Mbali na Nawali, baada ya kufungishiwa virago na Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Nuh alitua kwa mrembo mwingine shombeshombe ambaye hata hivyo hawakudumu

Imeandikwa na Global Publishers

0 comments:

Post a Comment