Msanii wa muziki Naj amekanusha tetesi za kugombana na mpenzi wake
Barakah Da Prince baada ya kudaiwa kupigiwa simu usiku wa manane na
aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Mr Blue.
Inadaiwa wakati Barakah ameshika simu ya mpenzi wake Naj, alipiga mtu
ambaye namba yake ‘iliseviwa’ Zai na baada ya Barakah kupokea alikuta
sio mwanamke bali ni mwanaume ambaye alidaiwa kuwa ni Mr Blue.
Akiongea katika kipindi cha U-Heard cha Clouds FM cha Jumatano hii, Naj
amekiri kusave kimakosa namba ya Mr Blue kwa jina la Zai.
“Kuna watu wanaongea vibaya lakini hawajui, kwanza mimi siwasiliani na
Mr Blue, unajua mimi mtu nikishakuwa naye hatuwezi kuwa marafiki,
mnakuwa marafiki mnaongea nini sasa,” alisema Naj.
“Na mimi zamani sana hata kabla sijaanza mahusiano na Barakah, nikapata
missed call kwenye hiyo namba, sasa mimi nikaisave ‘Zai’ kwa haraka
haraka ili niingie whatsapp ili nijue ni nani, kwa sababu mimi mara
nyingi nikipataga missed call sitakagi kumpigia mtu ambaye simjui, kwa
hiyo baada ya kufanya hivyo ndo nikamjua ni nani. Kwa hiyo ilikuwa
kitambo sana halafu mimi mwenyewe nilikuwa sijafuta wala nini na sio
kwamba ni namba ambayo naitumia wala nini,” alifafanua zaidi.
Pia Naj ameeleza jinsi mpenzi wake Barakah alivyoigundua namba ya Mr Blue kwenye simu yake.
“Nilimpa Barakah simu yangu akawa anaitumia hata sijui kati yao nani
alimpigia mwenzake kwa sababu namba ilikuwa kwenye majina. Kama
ningekuwa na mambo mengi nisingejiamini kumpatia simu mpenzi wangu, kwa
hiyo hata sijui nani alimpigia mwenzake kati yao, lakini namba ilitokea
kama Zai,” alisema Naj.
Hata hivyo hivi karibuni katika kipindi cha U-Heard, rapper Mr Blue
ambaye alifunga ndoa mapema mwaka huu na mwanadada aitwae Warda, alikana
kuwasiliana na Naj.
Home
»
Udaku
» Naj na Mr Blue wadaiwa kuwasiliana, Naj aeleza kwanini alisave namba ya Mr Blue kwa jina la ‘Zai’
Thursday, August 11, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment