Wakati wazazi wengi nchini wakihaha kudhibiti ulaji holela wa vitu
vitamu kwa watoto wao ili kuimarisha afya ya kinywa. utafiti mpya wa
hivi karibuni umeibuia mapya baada ya kubainika kuwa ulaji mzuri wa
chocolate unaweza kuongeza uwezo wa kufikiri na hivyo kutoa fursa kwa
watoto kufanya vizuri darasani.
Aidha, utafiti huo umebaini vilevile kuwa ulaji wa chocolate husaidia
kupunguza kasi ya kawaida ya kuzeeka kwa walaji itokanayo na kuongezeka
kwa umri. Ripoti ya utafiti huo ilitolewa hivi karibuni, inabebwa na
utambulisho usemao ‘ulaji wa chocolate huongeza utendaji kazi wa ubongo”
na kwamba ”unaweza kusaidia mtu kutozeeka haraka licha ya umri kuzid
kumtupa mkono’
Utafiti huo uliochapichwa mwezi huu katika jarida la Appetite, umebaini
kuwa kumbukumbu na uwezo wa kufikiria ufumbuzi wa mambo magumu kuwa
katika kiwango cha juu kwa watu wanaokula chocolate kwa wingi. Matokeo
hayo yameripotiwa kutoathiriwa na umri wa mlaji, uzito wa mwili wala
aina nyingine za ulinganifu wa jumla wa kiafya .
Inaelezwa zidi kuwa utafiti huo unaonyesha kuwapo kwa uhusiano mkubwa
kati ulaji wa kila mara wa chocolate na matokeo ya majaribio kuhusu
uwezo wa uubongo katika kufikiri hata hivyo utafiti huo haujathibitishwa
kwa asilimia 100 juu ya uhakika wa kisayansi juu ya kile
kilichobainishwa.
Aidhja imeonekana watu wanotumia zaidi chocolate walikuwa na lishe bora
zaidi na pia kunywa pombe kwa kiasi kidogo, na makundi yote yalitegemea
uwezo wa kukumbuka mambo kupitia kiwango chao cha ulaji wa Chocolate.
Sunday, August 28, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment